Habari zetu
Friday, June 26, 2015
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Mkuranga, Mkoani Pwani wamevamia tawi la Benki ya NMB na kuua Askari mmoja kisha kutokomea na fedha zote.
Update
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Jafary Mohamed, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa tukio hilo na kwamba sasa anajiandaa kwenda katika eneo la tukio.
"Ni kweli nimepata taarifa zenye maelezo machache kama hayo unayonieleza lakini niko kwenye ziara (Hakutaja ni ziara gani), ninajiandaa kwenda katika eneo la tukio, nikifika au kupata taarifa zaidi muda wowote kuanzia sasa nitawajulisha kwa kina" alieleza Kamanda Mohamed.
Subscribe to:
Comments (Atom)

